Said Ally aliyetobolewa macho na mtuhumiwa Scorpion maeneo ya Buguruni Sheli amekabidhiwa shilingi milioni 10 na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na kuhaidiwa kujengewa nyumba na kampuni ya GSM.

Makonda amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vitu alivyoviahidi Said Ally ana vipata pasipokuwa na shida yeyeto.

Akiongea leo katika kukabidhiwa pesa hizo mkuu wa mkoa amesema ‘Tumepata mdau ambaye amekubali na kumnunulia ndugu yetu Said nyumba, ambayo ni kampuni ya GSM na nimewambia wasikupeleke Magwepande, wasikupeleke Bunju, Mbagala, Gongo la Mboto.

Makonda aliendelea kusema “Nataka ukae mazingira yale yale ambayo umeyazoea. Iwe Tabata unakuja tena Buguruni, Mwenge. Nataka maeneo haya haya ambayo watu wamezoea kukuona. Kwahiyo ndugu zetu wa GSM wamekubali kuniunga mkono kumnunulia nyumba. Mi nakuombea neema ya bwana iendelee kutembea katika maisha yako,”.

Kwa upande wake, Said alishukuru na kusema, “Ukiona mtu anatoa chozi kwaajili ya mwananchi wake ni jambo zuri, alivyosikia kwenye vyombo vya habari hakuchelewa kuja. Lakini leo nashukuru sana kwa kila kitu alichonitendea, nashukuru sana.”

Pia Staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnum ametoa kiasi cha shilingi milioni mbili za kumkabidhi Said Ally.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *