Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli amekabidhiwa Bajaji mbili na kiongozi wa Bohra dunia Dk. Syedna Mufaddal Saifuddin ikiwa kama msaada wake kwa kijana huyo.

Kitendo hiko cha kukabidhiwa Bajaji hizo kimefanyika kwenye msikiti wa Mabohora uliopo maeneo ya Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alimuahidi Said Ally kumkabidhi bajaji mbili na piki piki tano pamoja na kununuliwa nyumba ya kuishi.

Wiki iliyopita Said alikabidhiwa shilingi milioni 10 na Makonda ikiwa ni ahadi yake ya kumsaidia kijana huyo aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli.

Wakati huo huo mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alimchangia Said shilingi milioni mbili.

Hii ni mara ya pili kwa kiongozi huyo mkubwa duniani wa Bohra kusaidia baadhi ya vitu nchini ikiwa ni siku chache zimepita tangu alipotoa msaada wa dola laki mbili na nusu kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya tetemeko la Kagera lililotokea mwezi uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *