Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa jitihada za kumpeleka Tundu Lissu Marekani kutibiwa zimeshindikana baada ya madaktari kutoridhia.

Lazaro Nyalandu ametoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook ambapo amendika ujumbe kuhusu kauli ya madaktari wanaomtibia Tundu Lissu jijini Nairobi Kenya, na kueleza kwamba madaktari hao wamesema hawawezi kuruhusu Tundu Lissu asafirishwe kupelekwa Marekani kutokana na hali yake jinsi ilivyo.

Kupitia akaunti yake ya Facebook Nyarandu ameandika “Kwa sasa mipango ya kumsafirisha Mheshimiwa Tundu Lissu nje itasimama kutokana na ushauri wa madaktari wa hospitali ya Nairobi, ili kuruhusu kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa hadi hapo itakavyoshauriwa au vinginevyo, ama endapo kutatokea umuhimu wa kufanya hivyo katika siku zijazo”.

Jana ana Lazaro Nyalandu alitoa taarifa kwamba wanafanya jitihada za kumpeleka Tundu Lissu Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi, huku wakisubiria ripoti ya madaktari wa hospitali ya Nairobi ambako mbunge huyo anatibiwa, na ndipo ilipokuja taarifa hiyo kwamba haitowezekana kumsafirisha kwa sasa.

Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma majira ya mchana, na usiku wa siku hiyo hiyo alikimbizwa jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu zaidi, kutokana na hali yake kutokuwa nzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *