Muigizaji wa Bongo movie ambaye pia n mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefungukia madai ya kutoka kimapenzi na msanii wa Muziki wa Dansi, Christian Bella kuwa hawezi kutoka naye na kwamba kazi za muziki ndizo zinamfanya kuweka mazoea naye.

Sabby anayetikisa katika Tamthiliya ya Talaka pamoja na Ngoma ya Inahusu amesema amekuwa akimposti Bella katika mitandao mbalimbali na kuwa naye karibu lengo likiwa kuonesha ‘alert’ ya kolabo naye mpya lakini wengi wameshindwa kuelewa na kumshambulia kukwa anabanjuka naye.

christian-bella

Muigizaji huyo amesema kuwa Bella ni kama kaka yake  na hawezi kutoka naye na haitatokea.

Ameongeza kwa kusema kikubwa ambacho wengi hawaelewi ni kwamba yupo mbioni kuibuka na ngoma mpya aliyomshirikisha hivyo wasubiri waone siyo kuhoji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *