Mwanamuziki wa hip hop nchini, Nikki wa Pili amesema kuwa sababu inayowafanya kutoweka wazi maisha yao binafsi wazi kwasababu hawahitaji familia zao kupata athari yatokanayo na muziki.

Nikki wa Pili amesema wamekuwa wakificha maisha yao binafsi kwa sababu hawahitaji familia zao au watu wao wa karibu kupata athari au madhara yanayotokana na kazi yao ya muziki.

 

Ameendelea kufafanua sababu ya kutenganisha muziki na mapenzi “Kwa hiyo kama mimi nakuwa nina mtu kwenye mahusiano siwezi kumleta katika huu ulimwengu wangu ambao kwanza una mambo mengi sana ambayo yanaweza kuharibu maisha yake, ndiyo maana sisi tumeamua kutenganisha muziki siyo tu na mapenzi bali na familia hata marafiki’.

 

Kwa upande wake G Nako yeye amesema kuwa wao wanaishi maisha simple na ya kawaida hawakami au kutaka kuonesha kila kitu kwa jamii ili jamii ijue. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *