Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema sababu ya jeshi hilo kushindwa kumkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu ni kutokana na kutopokea hati ya mahakamani Kisutu.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema sababu za Tundu Lissu hajakamatwa mpaka sasa ni kutokana na Polisi kutopokea hati yoyote kutoka Mahakamani Kisutu inayoagiza kukamatwa kwa Tundu Lissu lakini ikiwafikia tu watafanya hivyo.

Mbunge huyo na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama baada ya kutotimiza masharti ya Mahakama kwa kutohudhuria kwenye kesi yake inayomkabili Kisutu, Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu,  Dar es Salaam, Lisu na wenzake  walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *