Muigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Vincet Kigosi ‘Ray’ ameweka wazi sababu ya kutoishi na mpenzi wake Chuchu Hans ambaye amezaa nae mtoto mmoja.

Ray amesema kuwa sababu inayomfanya asiishi pamoja na mpenzi wake huyo ni mama yake mzazi hataki aishi mbali nae kwa hiyo inamlazimu aendelee kuishi kwao Sinza Mori.

Kuhusu Chuchu Hans kuishi kwa nyumbani kwa kina Ray, muigizaji huyo amesema kuwa kuna mambo hayakamilika kati ya mpenzi wake na mama yake mzazi kwenye maelewano.

wwe

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa ni kweli anaishi nyumbani kwao siyo kama hana nyumba ya kuishi ila mama yake hataki mkali huyo wa filamu ahame nyumbani kwao.

Ray amesema kuwa licha ya kuishi nyumbani kwake lakini amempangia nyumba mzazi mwenzie maeneo ya Sinza Darajani ili aishi nae kutokana na mama kumkataza kuhama kwao.

Kwa upande mwingine Ray amezindua sinema yake mpya ya ‘Gate Keeper’ ambayo alieleza kwamba imelenga kuvunja ukimya wake wa muda mrefu tangu alipofariki dunia, mshindani wake kwenye soko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *