Mbunifu wa mavazi maarufu Bongo, Martin Kadinda amesema kuwa anapata wakati mgumu kumsimamia Wema Sepetu kutokana na tabia zake zisizobadilika.

Martin Kadinda amesema kuwa licha ya Wema Sepetu kuwa mtu muhimu kwenye maisha na kazi zake amekuwa mtu ambaye habadiliki, hivyo inamuwia vigumu kumtengenezea mazingira mazuri ya kazi zake na kesho yake.

Kandika amesema kuwa ‘Changamoto kubwa kwake unajua Wema ni mtoto hakui, yani miaka inakwenda bado yuko vile vile, kikubwa ni kuweza kumtengenezea mazingira ili kesho na kesho kutwa aweze kuheshimika”.

Martin ameendelea kwa kusema ”Wema ana maisha yake binafsi, ana vitu vyake anavyovipenda kwa hiyo ninachokifanya zaidi ni kuweza dhibiti mambo yake binafsi yasimfanye kesho na kesho kutwa kushindwa kupata ugali wake wa kila siku”.

Kwa sasa Martin Kadinda amesimama kumsimamia msanii huyo kutokana na kubanwa na masomo huku akisema kwake atabaki kuwa msimamizi wa msanii huyo pale panapohitajika mchango wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *