Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kuungua kwa kikata umeme (socket breaker) katika kituo cha Ubungo , Dar es Salaam kinachotumiwa kudhibiti na kusambaza umeme mikoa yote ukiondoa Kagera na Kigoma katika Gridi ya Taifa, ndio chanzo cha kukatika kwa umeme jana na kuathiri mikoa mingine nchini.

Mikoa ya Kigoma na Kagera hupata umeme kutoka nchini Uganda.

Kaimu Meneja Mwandamizi, Mdhibiti Mifumo ya Umeme wa Tanesco, Abubakar Issa alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kukatika kwa umeme saa 12:32 asubuhi jana na kuathiri maeneo yaliyounganishwa kwa Gridi ya Taifa.

Ofisa huyo wa Tanesco alisema maeneo mengine yataendelea kurudishiwa nishati hiyo, kwa kuwa mafundi wa shirika hilo wanaendelea kushughulikia tatizo hilo ili kuhakikisha umeme unarudi katika hali ya kawaida kwa wote.

Akizungumzia hasara iliyopatikana baada ya kukatika kwa umeme, alisema bado wataalamu wa shirika hilo wanafanya tathmini ya hasara.

Kuhusu kukosekana kwa mvua katika mkikoa inayolisha mito katika mabwawa yanayozalisha umeme, alisema kwa sasa mabwawa yote yana maji ya kutosha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *