Mkali wa pop nchini Marekani, Justine Bieber uhenda asisafiri nchini Agrentina kutokana na kuhofia kukamatwa baada ya kumwagiza mlinzi wake kumpiga mmoja wa wapiga picha nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoenea zinasema kwamba Bieber hafikirii kukanyaga katika nchi hiyo kutokana na kitendo hicho huku akihofia uhenda akakamtwa na maofisa wa polisi au akafanyiwa fujo na mashabiki nchini humo.

Bieber anatarajia kufanya ziara yake ya kimuziki katika bara la Amerika ya Kusini lakini uhenda asiende katika nchi hiyo licha ya kuwa na mashabiki wengi nchini Argentina.

Mkali huyo alimuagiza mmoja wa walinzi wake kwenda kumpiga mpiga picha huyo baada ya kupiga picha ambapo staa huyo akupenda apigwe picha ndiyo akamuamuru mlinzi wake kwenda kutoa kichapo kwa paparazi huyo.

Justine Bieber ni mwanamuziki anayekumbwa na kashfa kibao kutokana na vituko vyake mwezi mmoja uliopita alishuka jukwaani katika jiji la Manchester wakatika wa show yake kisa mashabiki walikuwa wanapiga makelele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *