Sababu ya Ibrah kutofanya video na Joe Boy wa Nigeria

0
384

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ibrah amefunguka sababu za kushindwa kufanya video na msanii wa Nigeria Joe Boy ambaye amefanya naye wimbo iitwayo Wawa unaopatikana kwenye EP yake ya STEPS.

Ibraah ameeleza kuwa wakati msanii huyo anakuja Tanzania waliwasiliana ila alishindwa kufanya naye video kwa sababu alikuwa akishoot na msanii mwingine aitwaye Skiibii.

“Muziki ni Biashara huwezi jua yeye alikuwa na mipango gani na mimi nilikuwa na mipango gani wakati huo alipokuja hapa nchini.

Ibrah amesema kuwa Ila nilimcheki na niliwasiana naye kama brother na hata Airport nilikutana naye unajua sijawahi kuonana naye tulipiga story kama brother.

Kuhusu video lakini nilikuwa na Skiibii na wote walikuwa wamegongana siku, ikabidi nifanye video na Skiibii lakini soon naenda nchini Nigeria, kwa hiyo litakaa sawa na mashabiki zangu wakae tayari” ameongea Ibrah.

LEAVE A REPLY