Muigizaji wa Bongo Movie, Faiza Ally ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea sababu ya kumpenda mwanadada Mange Kimambi.

Faiza Ally ambaye amezaa na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuwa ameamua kuandika ujumbe huo ili watu wajue kama wawili hao wapo kwenye uhusiano mzuri.

Miezi kadhaa iliyopita wawili hao walitupiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mange Kimambi kumkashifu mrembo huyo.

Alichoandika Faiza Ally kwenye akaunti yake ya Instagram

“Watanzania mmenishanga ambavyo mnashangaa mimi kumpenda mange sasa labda niwape sababu zangu za msingi na mtambue mimi sio mfata mkumbo kama wengi wenu ambao mkiona mtu Ana tukanwa mnapiga makofi..mkiona mtu Ana zalilishwa mnapiga makofi..mkiona mtu anae endwa nanyi mnapenda yaani kifupi mbakua kama ngalawa zile boti zinaendaga na upepo au bendera hapana ! Na si kwamba nampenda kwa sababu msafi sana hapana Ana machafu yake ambayo nayachukia Tena sana na haina sababu kwamba nimchukie kwa sababu kuna vitu sivipendi Na si kwamba msafi sana Ana stahili kupendwa peke yake au labda nime muongo poa au nataka anipende au najioendekeza kwa namna yoyote ni sababu ambazo kwa Mtanzania mwenye akili atatambua kwa MANGE tunamhitaji Tanzania sana na kama vipi muombeeni sana maana ni muhimu kwenye nchi yetu kuwa na mtu kama mange mimi haya maneno siku anza kusema Leo hata wkt tunatukanana nilikua ni vitani tu lkn haina maana kwamba nilikua na chuki nae ….. sababu za msingi za Mimi ku penda mange…. 1: kwanza Ana akili : anatufungua maskio wengi na tu najua mengi kupitia yeye ambayo wengi tulikua hatuyajui na ni haki yetu kujua :3 nchi yetu inahitaji mtu kama mange wa kuweka kusimama na bila uoga kwa ajili yetu :4 mange ni mwema pamoja na yote maana anajitolea kwa wengi 5:ni shujaa kwa namna ya kipekee sana ! sasa mtu kama huyu mie namchukiaje moja kwa moja ??? Ktk swala zima la madawa na wauzaji anawatetea kina nani kama sis sisi ? Na ni kweli anayosema kwa sababu mitaani yako! Kama kuna Mtanzania anachukia sana mage basi hajajua side b ya mange ! Lkn siwezi kuwa muongo kusema kwamba yuko perfect kuna mambo ambayo siyapendi ! Kwanza pale ambapo anaingia personal life za watu na kuwazalilisha ! okay upande wangu alinizalilisha pia na Mimi nilimzalilisha lkn mchokozi alikua yeye na anajua! Any way mm ni raia wa kawaida tu na sijali! Lkn kwa mfano hata Kama makonda kadanganya na kufanya makonda utasa wake unahusiana nn ? Ukishataja muuza unga kuzalilisha familia yake inahusiana nn ? Au unapotukanana na mtu kuzalilisha na kuharibu kwa mababa zao kuna husiana nn? Kwa hiyo ndio vitu ambavyo sivipendi wala siungi mkono! Part 1”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *