Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka sababu zilizopelekea kuonekaza katika video ya wimbo wa Madee ‘Sema’ aliomshirikisha msanii Nandy.

Dogo janja ambaye ni anawakilisha kundi la Tip Top Connectiona amesema kuwa sababu kubwa ya yeye kuonekana kwenye video ya made ni kumfanya aendelee kuwepo zaidi kwenye muziki na kuonesha ubunifu katika muziki ili kutokuzoeleka.

Janjaro amesema kuwa Madee ameshaonekana sana kwenye video kwaiyo kitendo cha yeye kuonekana kwenye video yake ni kuzidi kumfanya awe karibu zaidi kwa mashabiki wake.

Pia Dogo Janja amesema kuwa kitendo hicho kitamfanya aendelee kuonekana kuwa bora kutokana na ubunifu wa video hiyo.

Madee amemtumia Dogo Janja kwenye kwenye video ya wimbo wake  na kuuvaa uhusika wa Madee  kitu ambacho ni kipya sana kwenye muziki wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *