Meneja wa mwanamuziki, Diamond, Sallam SK amefunguka sababu iliyosababisha Diamond kutohudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari, Iva Don yaliyofanyika nchini Uganda hapo jana.

Sallam SK amesema kuwa sababu iliyosababisha mwanamuziki huyo kutohudhuria mazishi hayo ni muingiliano wa ratiba ya Diamond na muda wa mazishi.

Meneja huyo amesema kuwa walitaka wahudhurie mazishi hayo jana alfajiri lakini ndugu walisafirisha mwili wa marehemu usiku kuelekea kijijini ambapo ndipo kulipofanyika mazishi.

Sallam SK amesema kuwa kutona na hayo wakashindwa kuhudhuria mazishi hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Kayunga nchini Uganda.

Marehemu Ivan Don enzi za uhai wake
Marehemu Ivan Don enzi za uhai wake

Pia Sallam amekanusha taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba wameshindwa kuhudhuria mazishi hayo baada ya kuzuiwa airport kuingia nchini Uganga kutoka na ishu za usalama.

Amesema wao walitaka kuhudhuria mazishi hayo kwaajili ya mkupatia pole Zari  kwa kuwa huyo ndiye  mtu wao.

Wiki iliyopita Diamond wakati akiwa jijini Nairobi nchini Kenya alisema kuwa atahudhuria mazishi hayo ili kumfariji  mpenzi wake Zari kwa kuwa ndiyo anamuhusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *