Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga ameelezea sababu za Diamond Platnumz kutokamatwa barabarani baada ya kuendesha gari huku akiwa ameachia usukani.

Kama Mpinga amesema kuwa Diamond kosa lake kubwa hakuwa amefunga mkanda na kuna wakati alikuwa akiachia usukani lakini utaona ni tofauti na wale vijana tuliowakamata.

Pia ameangeza kwa kusema kuwa kuachia usukani kwa sekunde kadhaa si kosa na ndiyo maana utaona hata kwenye matengenezo ya magari huwa kwenye kujaribu mtu anaachia kwa muda kuangalia kama gari litapoteza uelekeo au la.

Kuotka na sababu hizo jeshi hilo likaona kuwa Diamond ni kioo cha jamii na kitu alichokifanya ni kutofunga mkanda jambo ambalo ni kosa kisheria, ailimuita ofisini kwake kukiri kosa.

Kwa upande mwingine Kamanda Mpinga amezungumza kuhusu TRA kukamata gari barabarani, kutolewa matairi bodaboda zinazokatisha kwenye barabara za mwendokasi, viongozi wengi wa siasa kutotia sheria na mengine mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *