Mwanamuziki wa Bongo fleva, Belle 9 amesema kuwa sababu inayofanya wanamuziki wengi nchini kuimba nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi ni kutokana muziki wa aina hiyo kupendwa na watu wengi.

Belle 9 amesema kuwa sababu kubwa ya kutunga nyimbo za aina hiyo ni biashara kwa kuwa ujumbe huo ndiyo unaopendwa zaidi na mashabiki wa muziki kuliko ujumbe mwingine.

Mkali huyo amesema kuwa wanaimba nyimbo za mapenzi kwa sababu za kibiashara, ukiimba mapenzi ndiyo watu wanakuwa wepesi kupenda kuliko kuimba ujumbe mwingine.

Nyimbo nyingi ambazo ameimba Bell 9 zilikuwa na ujumbe wa mapenzi isipokuwa nyimbo yake ya ‘Nilipe Nisepe’ ambao ulikuwa na ujumbe tofauti.

Baadhi ya nyimbo hizo ni kama vile Sumu ya Penzi, Masogange, Burger Movie Selfie, Shauri Zao pamoja na Give It To Me.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *