Muigizajiwa Hollywood, Angelina Jolie amezua mjadala mkali alipokuwa akiitangza filamu yake mpya nchini Cambodia alipokaanga na kuwala buibui akiwa pamoja na watoto wake.

Angelina Jolie alipoulizwa sababu ya kula wadudu hao amesema kuwa bui bui ni wadudu wenye radha tamu sana.

Kula wadudu ni jambo lililohusishwa kwa muda mrefu na uigizaji katika vipindi vya runinga kama vile I’m a Celebrity… Get Me Out Of Here.

Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya watu duniani itafikia bilioni tisa ndipo tuweze kuwalisha, itabidi uzalishaji wa chakula uongezeke maradufu.

Idadi ya watu duniani inapoopanda, kuna juhudi za kutafuta njia mbadala za kupata chakula – hasa protini – badala ya vyakula vya kawaida kutoka kwa mifugo na samaki.

Grub wanaamini bado itachukua muda kwa watu kukubali kuwala buibui na nge kama alivyofanya Angelina Jolie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *