Kiungo wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs uhenda akarithi mikoba ya Bob Bradley katika klabu ya Swansea City baada ya kufukuzwa kwa kocha huyo.

Giggs alihusishwa mara mbili kuinoa klabu hiyo kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa Bob Bradley mwezi Oktoba mwaka huu.

Bradley aliachishwa kazi baada ya kuiongoza Swansea kwa siku 85 pekee na kuiacha katika nafasi ya 19 kwenye ligi.

Giggs alianza kufanya kazi na Manchester United chini ya David Moyes baada ya hapo akawa kocha msaidizi chini ya Louis van Gaal.

Taarifa zinadai kuwa Giggs amefanya mazungumzo na wasimamizi wa Swansea, na mwenyekiti wa klabu hiyo Huw Jenkins.

Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Rene Meulensteen amesema kuwa anaamini Giggs anatosha kuiongoza Swansea.

Wengine wanaosakwa na klabu hiyo ni meneja wa Wales, Chris Coleman kocha wa zamaniwa Leicester City, Nigel Pearson na aliyekuwa kocha wa Birmingham City, Gary Rowett.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *