Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Dk Getrude Rwakatare amechaguliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Sophia Simba.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Ramadhan Kailima akizungumzia uteuzi huo alisema CCM ilipeleka jina la Mchungaji Rwakatare ambapo walipitia fomu zake na kuridhika kuwa ana sifa za kuwa mbunge.

Sophia Simba ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) alifukuzwa uanachama wa chama hicho kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama Machi 11, mwaka huu.

Kutokana na kufukuzwa uanachama Sophia Simba akakukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Rwakatare anatarajia kuapishwa kuchukua nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *