Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amefunguka na kusema kitendo cha Tanzania kushindwa kutumia fursa ya kilimo cha umwagiliaji ni kitu ambacho kinamuumiza.

Rungwe amesema yeye angekuwa Rais wa nchi hii angehakikisha Watanzania wanalima mara nne kwa mwaka kwa kilimo cha kumwagilia na si kutegemea kilimo cha mvua.

Pia amesema kuwa Mungu ametujalia karibu kila kitu ila tunashindwa kutumia rasimali hizo jambo ambalo linatia aibu.

“Mimi ningemwagilia kwa kutumia ndege za kumwagilia maji mabuza yale ningemwagilia mashamba. lile bonde la Shinyanga pale mimi naona aibu sana, mimi ningehakikisha Watanzania wanafanya kazi wanalima kwa mwaka mara nne siyo lazima tulime mashamba nchi nzima bali tungelima mashamba ambayo yangetupa hadhi, nasema mimi ningefanikisha”.

Rungwe alikwenda mbali zaidi na kusema suala la kuhamisha maji ni jambo ambalo linawezekana na kutolea mfano nchi ambazo kiasili ni jangwa lakini saizi wanafanya kilimo baada ya nchi hizi kuchukua udongo sehemu nyingine na kupeleka kwao na kufanya kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *