Kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi ‘Singasinga’ na  mfanyabiashara James Rugemalira imehairisha leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni.

Kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye hakuwepo ilipangiwa Hakimu mwingine Cyprian Mkeha.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 31 mwaka huu, baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Washitakiwa hao wamerudishwa rumande hadi Agosti 31 kesi yao itakapotajwa tena kwa ajili ya kusikilizwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *