Mahakama ya Rufaa jijini Mwanza imehairisha rufani ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa Bunda Mjini ili kutoa nafasi kwa, Ester Bulaya kupata muda wa kujibu hoja za kisheria zilizotolewa na upande wa mkata rufani.

Rufani hiyo namba 199/216 ambayo leona ilikuwa isikilizwe na jopo la majaji watatu ambao wote walikuwepo mahakamani Augustine Mwarija, Rehema Mkuye na Mbarouk Salim, iliwasilishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Rufaa jijini Mwanza.

Kiongozi wa jopo la majaji hao, Jaji Salim amesema kesi hiyo inaweza kusikilizwa jijini Dar es Salaam au Mwanza ingawa hakusema itasikilizwa lini.

Wakili wa mleta maombi wa kwanza katika rufani hiyo (wapigakura wanne wa Bunda), Constatino Mtalemwa alisema rufani hiyo imefunguliwa baada ya kubainika kasoro za kisheria kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Musoma.

Wakili huyo amezitaja baadhi ya kasoro hizo ambazo zilisababishwa kukatwa kwa rufani hiyo ni kutoalikwa kwa mgombea wa CCM kwa wakati huo, Stephen Wasira kushiriki kwenye uhesabuji wa kura na mrufani wa kwanza Bulaya kutotoa ushahidi wa kutosha kama alitimiza masharti ya Sheria ya Uchaguzi Namba 6 ya Mwaka 2016.

Rufani hiyo kwa upande wa wakata rufani anatetewa na Wakili Mtalemwa na kwa upande wa mjibu rufani Bulaya inatetewa na Wakili Tundu Lissu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *