Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amefunguka na kusema kuwa si jambo la busara kwa mashabiki kusikiliza upande mmoja wa stori kuhusu yeye kukataa kushiriki kwenye video za ngoma ambazo ameshirikishwa.

Ruby amesema kuwa alikuwa hana haja ya kukataa kuonekana kwenye baadhi ya nyimbo ambazo yeye ameshirikishwa ila kuna wakati mwingine watu hao walikuwa wakimzingua.

Mwanamuziki huyo aliendelea kusema “Unajua ukisikiliza maneno ya upande mmoja unaweza kudhani labda kinachoendelea ni sawa mimi siwezi kukataa kufanya video zao sema muda mwingine unakuta wao ndiyo wanazingua, kuna muda mwingine mimi ndiyo nazinguliwa, watu wananikwamisha ili nisionekane kwenye hizo video”.

Kwa upande mwingine Ruby amewataka mashabiki zake wasahau mambo yoyote yaliyotokea kipindi cha nyuma na sasa amekuja kivingine na anaomba support kwa mashabiki.

Mkali huyo alietamba na nyimbo kama ‘Yule’ pamoja na ‘Forever’ sasa ameachia ngoma yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Wale Wale’ ambayo imetayarishwa na mtayarishaji Man Water kutoka Combination Sound.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *