Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amefurahishwa na maoni ya shabiki kwenye mtandao wa kijamii iliyosema kuwa Ruby ndiye aliyemfundisha muziki Kusah.

Maoni ya shabiki huyo aliweka kwenye posti ya Ruby ambayo alimtambulisha Wolper kama Manager wake mpya kwenye kazi zake za muziki na masuala mengine.

Komenti ya shabiki huyo ilisema kuwa Ruby ndiye aliyemfundisha Muziki Kusah na Ruby aliijibu comment ile kwa ishara ya kukubaliana na kile ambacho alikiandika shabiki huyo .

Shabiki huyo aliandika “Rubiiiivsaut ya busara bi kidude alimfundishabhadi kusah mziki saivi anajiona MTU bila rubby Nani angemjua” na Ruby akaijibu komenti hiyo kwa kuandika “ASANTE heeee kumbe sikua pekeangu kunawaliokua wanaona na kuelewa Mungu huyu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *