Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amefanikiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye msimu wa nne wa kipindi cha Coke Studio.

Ruby anaungana na wasanii wengine kutoka Tanzania pamoja na nchi nyingine kwenye msimu wa nne wa kipindi hicho cha Coke Studio kilichojizolea umaarufu barani Afrika bada ya kuwakutanisha wasanii mbal mbali.

Wasanii wengine wa Tanzania walioshiriki kwenye kipindi hicho kwa msimu huu wa nne ni pamoja na Joh Makini, Vanessa Mdee, Yamoto Band.

Huu ni msimu wa kwanza kwa Ruby kushiriki kwenye kipindi hicho ambapo ameungana na msanii wa Nigeria, Yemi Alade kutengeneza mchanganyiko wa nyimbo zao tofauti tofauti.

Ruby ni msanii mwenye kipaji cha kuimba kutokana na sauti yake kuwa kivutio katika soko la muziki wa Bongo fleva mpaka kupelekea kufanya vizuri kwa nyimbo zake alizowahi kuzitoa.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *