Staa wa movie za kibongo, Rose Ndauka  ametambulisha labo yake itakayowasimamia wasanii wa Bongo Fleva inayoitwa  ‘Ndauka Music’.

Katika tukio hillo Rose Ndauka pia amemtambulisha msanii wake mpya anayeitwa Kassim Casso ‘Casso’ ambaye anakuwa msanii wa kwanza kusainiwa katika lebo hiyo mpya inayomilikiwa na muzigizaji huyo wa Bongo movie.

Ndauka amesema kuwa ni muda mrefu amekuwa akitamani kusaidia vijana wenye vipaji lakini alikuwa anakwama kutokana na mambo yake kutomkalia poa lakini kwasasa amefanikisha jambo hilo.

Rose Ndauka ambaye pia ni mkurugenzi wa Ndauka Advert Limited ameeleza sababu ya kuingia kwenye muziki na si kuibua vipaji vya wasanii wa filamu amesema kuwa wasanii wa filamu ameshawaibuwa na sasa ni zamu ya muziki.

Kwa upande wake msanii huyo mpya wa Ndauka Music, Casso ameishukuru lebo yake hiyo kwa kumsaini pamoja na kuwaahidi mashabiki kuachia kazi nzuri.

Rose Ndauka anaungana na wasanii wenzake wa Bongo movie walionzisha lebo ya muziki ambayo ni Shilole pamoja na Wema Sepetu ambao pia wana lebo zinazosimamia wasanii wa Bongo fleva.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *