Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney ameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya Europa ligi dhidi ya Feyenoord kesho.

Mshambuliaji huyo amefanya mazoezi na timu hiyo leo asubuhi lakini kocha wake Jose Mourinho ajamjumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 20.

Vile vile kuna wachezaji hawakufanya kabisa mazoezi na timu hiyo kutokana na sababu tofauti ambao ni  Antonio Valencia, Luke Shaw and Jesse Lingard, Henrikh Mkhitaryan naPhil Jones.

Kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho ametaja kikosi cha wachezaji 20 watakao safairi na timu kuelekea Uholanzi kwa ajili ya mechi hiyo ya Europa ligi itakayochezwa siku ya Alhamisi.

Wachezaji watakaosafiri na timu ni De Gea, Romero, Johnstone; Darmian, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling; Carrick, Fellaini, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young; Ibrahimovic, Martial na Rashford.

Manchester United imepangwa kundi A pamoja na timu za Fenerbahce ya Uturuki, Zorya ya Ukrane na Feyenoord ya Uholanzi ambapo mechi zao zinatarajia kuanza kesho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *