Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney leo anatarajia kucheza mechi ya kombe la FA dhidi ya Reading raundi ya tatu ya Kombe hilo.

Rooney amekosa mechi tatu za Ligi Kuu kipindi cha sikuu ambazo United ilishinda zote baada ya kupata majeraha ya misuli ya paja kwenye mazoezi siku ya Krismasi.

Kocha wakeJose Mourinho amebainisha kuwa wachezaji hao watacheza katika mechi hiyo itakayopigwa katika uwanja wa Old Trafford, akiongeza kuwa ana kikosi kipana cha kufanya uchaguzi.

Rooney atakuwa anaifukuzia rekodi ya muda wote ya kufunga magoli na huenda akapata fursa ya kuifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton mbele ya legendari huyo wa Mashetani Wekundu anayetarajiwa kuushuhudia mchezo huo.

Luke Shaw pia atakuwepo baada ya wiki kadhaa za kupambana kurejea kwenye afya yake na Daley Blind pia atakuwepo kwa mara nyingine baada ya kuikosa West Ham na kipa wa ziada Sergio Romero ataanza katika mchezo wa leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *