Mshambuliaji wa Uingereza na Manchester United, Wayne Rooney amesema ataendelea kuchezea timu ya Taifa ya Uingereza, licha ya kuondoshwa katika kikosi kilichanza jana dhidi ya Slovenia kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2018.

 

Rooney aliyecheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita, na Uingereza kushinda 2-0 dhidi ya Malta amesema kwa sasa ndiyo kwanza ana umri wa miaka 30 na angependa kucheza hadi akiwa na umri wa miaka 40 kama alivyokuwa winga wa Wales Ryan Giggs.

 

Rooney amekuwa akikosolewa kiwango chake kushuka kadri siku zinavyokwenda, na awekwa benchi na kocha Jose Mourinho kwenye kikosi cha Manchester United.

 

Nahodha huyo wa timu za Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, amefunga bao 1 pekee kwenye michezo 12 kwa klabu yake pamoja na Timu ya Taifa msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *