Nahodha wa Manchester United na Uingereza, Wayne Rooney ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Rooney amezungumza hayo mbele ya waandishi wa habari kwenye mouton wa kwanza baada ya kocha wa Uingereza, Sam Allardyce kumthibitisha kuendelea na unahodha wa Uingereza.

Rooney amesema kwamba kombe la dunia Urusi mwaka 2018 ndiyo itakuwa mwisho wa kuicheza Uingereza huku akisema miaka miwili iliyobakia atahakikisha timu hiyo inafuzu kucheza kombe hilo la dunia.

Mshambuliji huyo wa Manchester United ameichezea Uingereza jumla ya mechi 115 mpaka sasa na kufanikiwa kushinda magoli 53.

Kama Rooney akicheza mechi ya jumapili dhidi ya Slovakia ya kufuzu kombe la dunia atakuwa amevunja rekodi ya David Beckam kucheza mechi nyingi kwenye kikosi cha Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *