Nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza, Wayne Rooney amesema kuwa kwasasa anapitia kipindi kigumu baada ya kocha wa muda Southgate kuthibitisha hatoanza kwenye mechi ya leo dhidi ya Slovania.

Kocha wa muda wa Uingereza, Gareth Southgate amesema uamuzi huo umekuja baada ya kujadiliana na mcheaji huyo ambaye kwasasa anaonekana kiwango chake kushuka ghafla.

Rooney alionesha kiwango kibovu mbele ya mashabiki wa timu hiyo kwenye mechi dhidi ya Malta iliyofanyika katika uwanja wa Wembley na Uingereza kushinda 2-0.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Manchester United ameanzia benchi mechi tatu za klabu yake baada ya kiwango chake kutomridhisha kocha wake Jose Mourinho.

Southgate amesema kuwa Rooney ataendelea kubakia nahodha wa timu hiyo lakini kwenye mechi ya leo nahodha atakuwa kiungo wa klabu ya Liverpool, Jordan Henderson ambaye kwasasa anaonekana kuwa na kiwango bora.

Rooney ametangaza kusataafu soka la kimataifa mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Urusi ameichezea Uingereza mechi 117 na kushinda magoli 53 na kushika rekodi ya kucheza mechi nyingi kuliko mchezaji yeyote anayecheza nafasi ya ndani huku rekodi ya jumla ikishikiliwa na Peter shilton aliyekuwa golikipa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *