Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ameondolewa katika kikosi kitakachomenyana na Chelsea katika hatua ya robo fainali kombe la FA itakayopigwa leo hii.

Rooney aligongana na mlinzi Phil Jones wakati wa mazoezi na kupata majeraha katika mguu wake, huku Zlatan Ibrahimovic akianza kutumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu baada ya kumpiga kiwiko mlinzi wa Bournemouth Tyrone Mings.

Washambuliaji Anthony Martial na Marcus Rashford nao pia watakosa mchezo huo kwa kuwa ni wagonjwa.

Manchester united hawatakuwa na mshambuliaji wa kikosi cha kwanza leo kutokana na wachezaji wao kuwa majeruhi.

Kwa upande wa kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema wachezaji wa kikosi chake wote ni wazima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *