Naodha wa Manchester United na Uingereza, Wayne Rooney amemuomba radhi kocha wake Gareth Southgate baada ya picha kutolewa zikimuonesha akiwa amelewa wakati wa sherehe ya harusi.

Nahodha huyo alihudhuria sherehe hiyo ya harusi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa imeweka kambi wakicheza mechi ya kimataifa.

Rooney amesema ingawa picha hizo zilipigwa wakati wake wa kupumzika alkini si nzuri kusambazwa kutokana na hadhi yake.

Gazeti la The Sun la Uingereza lilichaisha picha hizo ambazo zinamuonesha Rooney akiwa kwenye sherehe usiku wa Jumamosi baada ya mechi ya England ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.

Chama cha Soka cha England (FA) kimesema kitatathmini upya sheria kuhusu mambo ambayo wachezaji wanaruhusiwa kufanya wakati wa mapumziko.

Rooney hakucheza mechi ambayo England walitoka sare 2-2 na Uhispania Jumanne kwa sababu ya jeraha ndogo kwenye goti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *