Naodha wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kwamba anatarajia kuiona Manchester United ya zamani ikirudi tena chini ya kocha mpya Jose Mourinho.
Mourinho ambaye amechukua nafasi ya kocha Louis Van Gaal klabuni hapo tayari ameshasajili wachezaji watatu mpaka sasa ambao ni Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.
Rooney amesema kwamba kwasasa klabu hiyo ipo vizuri kutokana na wachezaji waliowasajili kwahiyo wanaweza kuleta upinzani kwenye ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi Agosti.
Manchester United ambao ni mabingwa wa kombe la  FA wanatarajiwa kuanza kutupa karata yao ya kwanza watakapopambana dhidi ya mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, Leicester City kwenye mechi ya ngao ya jamii siku ya jumapili.
Vile vile Rooney ameongeza kwa kusema kama Manchester United wakimpata kiungo wa Juventus, Paul Pogba itakuwa vizuri sana kwasababu atashirikiana vizuri na mshambuliaji mpya Zlatan Ibarahimovic.