Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney amefikia rekodi ya mabao ya Sir Bobby Charlton ambaye aliweka rekodi ya kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao katika klabu ya Manchester United.

Rooney  amefikia rekodi hiyo baada ya kushinda goli kwenye mechi ya kombe la FA kati ya Manchester United na Reading na kufikisha jumla ya mabao 249 katika mechi 543.

Rekodi hiyo Bobby Charlton ameiweka tangu mwaka 1973 alipokuwa anachezea klabu ya Manchester United.

Mwaka 2015 Rooney alivunja rekodi ya Charlton ya mabao 49 aliyofungia timu ya England na kuongeza idadi hiyo hadi mabao 53.

Wakati wa mechi yake ya kwanza alipoihama Everton kwa kima cha pauni milioni 27 mwaka 2004 alifunga bao dhidi ya Fenerbahce.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *