Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana amefunga hat-trick yake ya 50 tangu aanze kucheza soka ya kulipwa huku Real Madrid kwenye ushindi wa 6-3 dhidi ya Girona.

Ronaldo alifunga krosi ya Toni Kroos lakini kichwa cha Cristhian Stuan kilifsawazisha na kufanya mambo kuwa 1-1

Stuani alifunga bao la pili la Girona, Gareth Bale alifunga la tano , kabla ya Juanpe kuifungia Girona bao la tatu lakini Ronaldo alipata bao lake la nne na la sita katika muda wa majeruhi.

Matokeo hayo yanaiweka Real Madrid juu ya Valencia lakini wako pointi nne nyuma ya Atletico Madrid ambao walilazwa 2-1 na Vilareal.

Real wako pointi 15 nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona ambao walishinda 2-0 dhidi ya Athletico Bilbao siku ya Jumapili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *