Mshambulijai wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya ukwepaji kodi kiasi cha doa za kimarekani milioni 16.5.

Waendesha mashtaka wamedai kuwa kodi ni kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014 na inahusu mapato ya nje na uwanja na haki za picha zake

Nyaraka zilizovuja zilieleza kuwa Cristiano Ronaldo amekwepa kodi kutokana na kipato chake kuwekwa kuwekwa kwenye akaunti za nje ya hispania

Ronaldo amekana shutuma hizo huku msemaji wa wakala wa mchezaji huyo alisema mwezi uliopita kuwa mchezaji huyo hakuwa na chochote cha kuficha.

Kisa hiko kinafananishwa na kisa cha mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ambaye alikutwa na kashfa kama hiyo ya Ronaldo na ukwepaji kodi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *