Ronaldo, Bale na Griezmann nani kuwa mchezaji bora Ulaya?

0
406

 

Wachezaji, Gareth Bale wa Real Madrid na Wales, Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na Ufaransa na Cristiano Ronaldo wa Real Mdrid na Ureno wamechaguliwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora barani Ulaya msimu wa mwaka 2015/16.

ronaldo

Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa siku ya Alhamisi wakati wa upangaji wa makundi ya klabu bingwa barani Ulaya mjini Monaco nchini Ufaransa.

Wachezaji hao wamepigiwa kura kutoka kwa waandishi wa habari ambao ni wanachama wa EUFA ambapo waliopiga kura hizo walikuwa 55.

bale

Msimu uliopita mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi alishinda tuzo hiyo ambapo mwaka huu aliingia kwenye listi ya wachezaji waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo lakini hakufanikiwa kuingia hatua ya mwisho.

man

LEAVE A REPLY