Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ametoa bei itakayo tumika kununulia perfume yake ya ‘CR7 Eau de Toilette’.

Bei ya reja reja itakua ni kiasi cha Pound £19 sawa na shilingi 56219 kwa pesa za Tanzania huku ikiambatana na boksi lenye Aftershaves, Shower Gels na Deodorants.

Ronaldo akiwa na perfome yake aliyozindua juzi.
Ronaldo akiwa na perfome yake aliyozindua juzi.

Ronaldo ametambulisha rasmi bidhaa yake mpya ya Perfume aliyoipa jina la CR7 Eau de Toilette, ikiwa ni perfume ya tatu kwenye orodha ya manukato yake, ambapo kuna Cristiano Ronaldo Legacy na Cristiano Ronaldo Legacy Private Edition.

Mbali na mpira mchezai huyo amekuwa mjasiliamali wa bidhaa mbali mbali zinazomfanya azidi kuwa tajiri kwa wanamichezo duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *