Staa wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Ulaya kwa msimu wa 2015/15 katika sherehe zilizofanyika nchini Ufaransa.

Ronaldo ametwaa tuzo hiyo akiwabwaga, Gareth Bale wa Real Madrid pia na Antoine Griezmann w Atletico Madrid waliofikia hatua ya tatu bora.

Kwa mujibu wa kura 55 zilizopigwa, Ronaldo amepata kura 40, akifuatiwa na mfaransa Antoine Griezmann aliyepata kura 8, huku Gareth Bale raia wa Wales akiambulia kura 7 pekee.

Zoezi la upigaji kura liliwashirikisha waandishi 55 wa habari za michezo kutoka nchi wanachama wa UEFA.

Baadhi ya mambo yalichongia Ronaldo kupata tuzo hii ni pamoja na ubingwa wa michuano ya Ulaya kwa ngazi ya vilabu ambapo aliiongoza Real Madrid kutwaa kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) kwa msimu huo, kabla ya kuiongoza timu yake ya Taifa ya Ureno kutwaa kombe la Mataifa ya Ulaya UEFA EURO 2016.

Mara ya pili kwa Ronaldo kutwaa tuzo hiyo baada ya kufanya hivyo katika msimu wa 2013/14.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *