Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kiume kwa mara ya pili mfululizo.

Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Alipokea tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.

Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.

Aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro kwa wanawake mwaka 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *