Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano ameshinda ya mwanasoka bora wa Ureno zilizotolewa na shirikisho la soka la Ureno.

Ronaldo, 33, ameshinda tuzo hiyo mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo kwa kuwabwaga wachezaji wenzake wengine wa Ureno akiwemo Bernardo Silva (Manchester City) na golikipa Rui Patricio (Sporting CP).

Kwa upande wa Mourinho ameshinda tuzo ya Vasco de Gama kutokana na kufanya kazi yake kwa ubora na majukumu yake kama ubalozi wa Ureno.

Wakati huo huo kocha wa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa, Leonardo Jardim ameshinda tuzo ya kocha bora kwenye upande wa soka wa wanaume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *