Mshambuliaji wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kupata watoto mapacha.

Ronaldo amethibitisha kupata watoto hao baada ya kutolewa nje kwa timu yake ya Ureno dhidi ya Chile kwenye michuano ya kombe mabara yanayoendelea nchini Urusi.

Siku nne zilizopita vyombo vya habari nchini Ureno vilitangaza kuwa pacha wake walizaliwa kutoka kwa mama aliyejitolea kushika mimba kwa niaba ya mkewe nchini Marekani.

Lakini ni baada ya timu yake kuondolewa katika mashindano hayo kwa njia ya penalti na chile ndiposa akathibitisha kuzaliwa kwa pacha hao.

Kupitia akaunti yake facebook ameandika “Nina furaha chungu nzima,hatimaye kuwa na watoto wangu kwa mara ya kwanza.

Tayari ana mwana wa kiume, Cristiano Ronaldo Junior ambaye alizaliwa mnamo mwezi Juni 2010.

Licha ya kupata watoto hao mapacha, mpenzi wake Ronaldo ambaye ni mwanamitindo wa Uhispania Georgina Rodriguez amethibitika kuwa na ujauzito wa miezi mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *