Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi baada ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya nne.

Nafasi ya tatu imeshikwa na mshambuliaji wa Ufaransa na Atletico Madrid Antoine Griezmann.

Ronaldo ameisaidia Real Madrid kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita pamoja na kuisadia ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya mwaka huu.

Mchezaji huyo ameshinda tuzo hiyo kuanzia mwaka 2008, 2013, 2014 na 2016 mara zote akichuana na mpinzani wake Lionel Messi.

Baada ya kutangazwa Ronaldo amesema kuwa hakufikiria katika maisha yake kama angeshinda tuzo hiyo kwa mara ya nne.

Ronaldo amewashukuru wachezaji wenzake timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid kwa ushirikiano wanaomuonesha wakati wa mechi zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *