Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza duniani kufikisha  followers milioni 100 katika mtandao wa Instagram.

Aliandika historia nyingine wiki hii, baada ya kufunga hat-trick yake ya 47 katika uchezaji wake wa soka ya kulipwa.

Mchezaji huyo kutoka Ureno pia ana mashabiki wengi zaidi kwenye Instram kuliko mwanamume mwingine yeyote yule.

Ndiye wa sita katika kufuatwa na watu wengi zaidi mtandao huo duniani kutokana na idadi ya mashabiki alionao kwasasa.

Wanaomzidi pekee ni Beyonce, Taylor Swift, Ariana Grande, Selena Gomez na akaunti yenyewe ya Instagram.

Ronaldo ana wafuasi wengi kuwashinda Kim Kardashian, Jenner, Justin Bieber na Dwayne ‘The Rock’ Johnson.

Katika soka, anayemfuata ni nyota wa Barcelona Neymar ambapo anafollowers 74m kwenye mtandao huo.

Lionel Messi anafollowers 71m huku David Beckham akiwa na followers 36m na James Rodriguez akiwa na followers 30m.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *