Mchezaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameandaa nyumba yenye thamani ya Sh bilioni 13 kwa ajili ya kufikia watoto wake mapacha watakaozaliwa hivi karibuni.
Ronaldo anatarajia watoto hao kutoka kwa mpenzi wake Georgina Rodriqueza mbaye ni mwanamitindo maarufu nchini Uhispania.
Pia Ronaldo amethibitisha kuweka vito mbalimbali vya thamani kwenye nyumba hiyo kwa ajili ya watoto hao.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kwa jina la Cristiano Jr, ujio wa watoto hao utaongeza ukubwa wa familia yake lakini kwa mchumba wake huyo mwenye umri wa miaka 23 itakuwa ndio watoto wake wa kwanza.
Kupitia akaunti ya Instagram, Georgina amedai kuwa familia hiyo kwa sasa ipo katika furaha kubwa ikiwa inatarajia kupata watoto hao wawili.
Mwanamitindo huyo ameandika “Muda mfupi ujao familia itakuwa kubwa na Cristiano Jr. anatarajia wadogo zake wawili, tuna furaha mno,”.