Hat-Trick ya Christiano Ronaldo imeisadia timu yake ya Real Madrid kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uhispania katika uwanja wa Vicente Calderon.

Ronaldo amenza kuipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 23 baada ya kupiga mkwaju wa faulo na kumshinda kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak na kutinga nyavuni.

Goli la pili Ronaldo alifunga katika dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Atletico Madrid, Savic kumuangusha Ronaldo eneo la hatari.

Ronaldo alimaliza hesabu ya magoli kwa kushinda goli la tatu katika dakika ya 77 baada ya kupokea pasi kutoka kwa winga Galeth Bale.

Kwa matokeo hayo Real Madrid inaongoza kwa kuwa na alama 30 baada ya kucheza mechi 12 nyuma ya wapinzani wao Barcelona ambayo ina alama 26 baada ya kutoka sare 0-0 dhidi ya Malaga jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *