Winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ametoa kiasi cha euro milioni tatu ikiwa ni rambi rambi yake kufuatia vifo vya wachezaji wa klabu ya Chapecoense ya Brazil.

Klabu hiyo ya Brazil ilipata ajali ya ndege kwenye milima ya Medlin nchini Colombia wakati ilipokuwa inakwenda kucheza mechi ya kombe la Sudamericana dhidi ya Atletico National.

Mchezaji huyo ameamua kuchangia kiasi hicho kwa timu hiyo kama mchango wake baada ya kuguswa na msiba huo uliogusa meadani ya soka duniani kwa ujumla.

Mwaka jana Ronaldo aliwahi kuchangia kiasi cha paundi milioni 5 kwa wananchi wa Nepal waliokumbwa na mafuriko.

Msiba huo umegusa watu wengi dunia hususani wachezaji mpira baada ya baadhi ya wachezaji kuelezea hisia zao kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *