Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter limetikisa eneo la Umbria katikati mwa Italia na kufukia watu chini ya vifusi.

Tetemeko hilo lilitokea mida ya saa tisa na dakika thelathini na sita usiku, 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi.

Mtetemeko ulisikika katika miji ya mbali kama vile Roma na Italia.

Mji wa Roma baadhi ya nyumba zilitikisika kwa sekunde 20 kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica nchini humo.

Watu wanne wameripotiwa kufariki katika eneo la Accumoli na meya wa mji jirani wa Pescara del Tronto amesema watu wawili wazee walifariki baada ya nyumba yao kuporomoka.

Mwaka 2009 tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 lilitokea eneo la Aquila na kusikika pia katika mji wa Roma ambapo watu zaidi ya 300 walifariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *