Wanamuziki wa hip hop, Roma Mkatoliki na Moni pamoja na wenzao 2 leo wanatarajiwa kueleza sakata zima la tukio la kutekwa kwao siku ya Jumatano.

Roma na wenzake leo wanatarajia kukutana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuelezea nini kilitokea mpaka wanamuziki hao wakatekwa na watu wasiojulikana wakati wakiwa studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuruhusiwa kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam na kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Mwananyamala, Roma aliwaambia waandishi wa habari kwamba atazungumza leo kuhusu sakata zima la kutekwa kwao.

“Mi ni mzima kabisa, nipo vyema kiafya na kiakili na wenzangu watatu nikimaanisha Mon, Bin Laden prodyuza wetu pamoja na Imma mfanyakazi wetu pale Tongwe; wote tu wazima tunaendelea vizuri, kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa za tukio zima ambavyo limetokea.

“Lakini taratibu hizo zinatufunga tusiweze kuongea chochote kwa sasa hivi, lakini ratiba naweza kuwapa kushinda kesho Jumapili, Jumatatu nadhani ndiyo kutakuwa na ‘Press Conference’ kukutana na kuongelea kuhusu hiyo stori, mturuhusu tu tukapumzike nawashukuru, niseme tu asante,”.

Roma na wenzake walitekwa Jumatano wiki hii wakiwa katika studio za Tongwe Recods iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *